8 Oktoba 2014 Imebadilishwa mwisho saa 08:32 GMT
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania hii leo anataraji kukabidhiwa katiba rasmi iliyopendekezwa mjini
Dodoma.
Tukio hilo la kihistoria linahitimisha mchakato wa kikao cha Bunge maalum la Katiba kilichomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuipitisha katiba
tarajiwa kwa zaidi ya theluthi mbili ambapo kwa sasa inasubiri kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni hapo mwakani.
Huku katiba hiyo mpya iliyopendekezwa ikitarajiwa kuwasilishwa kwa rais baadaye hii leo, suala la kutojumuishwa moja kwa moja kwa mahakama ya
kadhi katika katiba hiyo linaendelea kuwakera baadhi pamoja na serikali kuahidi kuliwasilisha bungeni kwa majadiliano zaidi hapo baadaye.
Chapisha Maoni