RAIS wa Zanzibar na Mweneykiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Mh. Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee, Dkt Shein
amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 55(1) cha Katiba ya Zanzibar ya
mwaka 1984.
Mheshimiwa Said Hassan anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mh. Othman Masoud Othman ambaye Uteuzi wake
umefutwa kwa mujibu wa Vifungu vya 53, 54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungu
12(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
Kabla ya Uteuzi huo Mheshimiwa Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar. Uteuzi huo umeanza tarehe 07, October,
2014IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Chapisha Maoni