SHIRIKISHO la Muziki Tanzania limetoa pongezi za dhati kwa Bunge Maalum la Katiba lililokuwa likiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe.
Samuel Sitta kwa kuingiza Ibara tatu katika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa huko mjini Dodoma.
Pongezi hizo zilitolewa jana na Rais wa Shirikisho hilo Bw. Addo November alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari hapo jana huku akisema kuwa
Rasimu Inayopendekezwa imezingatia haki za Wasanii kwa kuingiza Ibara tatu zikiwemo Ibara ya
15, ya 38 (II) na Ibara ya 56, 3 (e) ambazo Ibara hizo
zinalinda kazi za muziki na sanaa zote kwa ujumla.
(Martha Magessa)
Bw. November alieleza kuwa Shirikisho limefurahi kuona kuwa Sheria ya inayohusu masuala ya kazi za
sanaa katika nchini imeanza kutekelezwa Kikatiba kama ilivyo katika nchi mbalimbali zikiwemo
Marekani, Rwanda na Uingereza.
"Kwa kubainisha ibara hizi katika Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa, zinaonyesha ulindaji wa Hati Miliki
(Intellectual property) za Wasanii na kazi zao na hii itasaidia kuboresha maisha ya wasanii kimapato kwa kupitia kazi zao kwani Katiba hii itawalinda wasanii
Kisheria", alisema November.
Aliongeza kuwa Shirikisho limeingia Mkataba na Kampuni ya JB Belmont kwa kuweza kuwapatia wasanii na waandishi wa habari punguzo la bei
katika huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
Aidha, November aliwashauri waandishi wa habari kuunda Shirikisho la Waandishi wa habari la muziki
kwani hii itasaidia kupata na kutoa taarifa mbalimbali
kwa jamii zinazohusu masuala ya muziki kwa kuaangalia walikotoka na wanakoelekea kimaendeleo.
Naye Meneja Mahusiano wa Kampuni ya JB Belmont, Bi. Gillian Macheche alisema kuwa kutakuwa na
punguzo la asilimia 40 kwa huduma mbalimbali ikiwemo kukodi Ukumbi wa Mkutano, Vyumba vya kulala wageni, vyakula na Vinywaji kwa wasanii na
waandishi wa habari.
Kwa upande mwingine Mjumbe wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mwanamuziki mkongwe nchini Bw.
Kassim Mapili alitoa shukrani zake za dhati kwa waandishi wa habari kwa kutoa taarifa kwa umma juu
ya afya yake pamoja na jamii kwa ujumla kwa kumsaidia katika kipindi chote alichokuwa akitibiwa
ugonjwa wa Moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Chapisha Maoni