0
MASHABIKI wa Manchester United
wamemchagua kipa David de Gea kuwa
Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa klabu hiyo, baada ya Mspanyola huyo kupata asilimia 70 ya jura zilizopigwa kwenye mtandao.

Licha ya kushindwa kuzuia nyavu zake
kutikiswa katika mchezo wowote mwezi huo, De Gea alikuwa katika kiwango kizuri wakati United ikiifunga Everton kabla ya kutoa sare na West Brom ugenini na baadaye na vinara
wa Ligi Kuu England, Chelsea nyumbani.

Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 23 alipangua mkwaju wa penalti Leighton Baines na kuokoa michomo miwili ya hatari ya The Toffees dakika za mwishoni, kuiwezesha timu ya Old Trafford kupata pointi moja, kabla ya kuokoa mchomo mwingine wa
Eden Hazard wakati Mbelgiji hjuyo alipopata nafasi nzuri ya kufunga timu hiyo ikitoka 1-1 na kikosi cha Jose Mourinho.

Chapisha Maoni

 
Top