CHELSEA imeichapa mabao 2-1 Liverpool Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
Aliyeipa pointi tatu za leo Chelsea ni
mshambuliaji wa Hispania, Diego Coasta
aliyefunga bao la ushindi dakika ya 67,
akimalizia kazi nzuri ya Cesar Azpilicueta.
Emre Can alitangulia kuifungia Liverpool
dakika ya tisa, kabla ya Gary Cahill
kuisawazishia Chelsea dakika ya 14 .
Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet,
Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno, Gerrard, Can/Allen dk70, Henderson, Coutinho/Borini dk70, Sterling na Balotelli/Lambert dk79.
Chelsea: Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry,
Azpilicueta, Matic, Fabregas, Ramires/Willian dk54, Oscar, Hazard/Luis dk90, Costa/ Drogba dk90.
Chapisha Maoni