Pande mbili zinazopigana Sudan Kusini zimepewa siku 15 zaidi kumaliza vita vya karibu mwaka, na kuhitimisha makubaliano ya kugawana madaraka.
Iwapo hazikufanya hivyo, basi pande hizo mbili zitawekewa vikwazo na mataifa mengine ya Afrika
Mashariki.
Msemaji wa Jumuia ya nchi za Pembe ya Afrika, (IGAD) alieleza kuwa baada ya mazungumzo ya siku mbili mjini Addis Ababa, pande zinazopigana
Sudan Kusini zimekubali kusitisha vita moja-kwa- moja.
Pande hizo zilionywa yatayofwata iwapo zitavunja makubaliano, kama alivotamka msemaji wa IGAD.
"Makubaliano ya kusitisha mapigano yakivunjwa na upande wowote ule, hatua zinazofuata zitachukuliwa na Jumuia ya IGAD: Mali za pande hizo zitazuwiliwa.
Wanasiasa watapigwa marufuku kusafiri katika eneo la IGAD Silaha na risasi zitazuwiliwa kupelekwa Sudan
Kusini, pamoja na zana zote zinazoweza kutumiwa kwenye vita"
Chapisha Maoni