0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete jana, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia
ya wananchi mbali mbali nchini kujibu
ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa
kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya
haraka ambao amekuwa anatumiwa na
wananchi tokea mwishoni mwa wiki.

Tangu alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) Jumamosi iliyopita kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia nafuu ya haraka.

Rais Kikwete bado anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia SMS
Rais Kikwete waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu anakusudia kujibu SMS zote ambazo ametumiwa.

Aidha, Rais Kikwete jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania kwa mara ya kwanza tokea afanyiwe upasuaji.

Rais alizungumza na Makamu wa Rais
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal,
Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.

Wakati huo huo, madaktari wanaondelea
kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa
bandeji kwenye sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali yake inaendelea vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiwasiliana na baadhi ya wananchi
waliokuwa wakimjulia hali kupitia simu
yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms) leo Jumatatu.Rais Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns Hopkins
jijini Baltimore Maryland nchini Marekani
anaendelea vizuri na anafanya mazoezi
mara kwa mara na afya yake inaendelea
kuimarika(picha na Freddy Maro)
Mwisho.


Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Novemba,2014

Chapisha Maoni

 
Top