Msichana Kulwa Joseph (21) mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) mkazi wa kijiji cha usonga kata ya sirambo wilayani kaliua mkoani Tabora, amenesurika kuuawa na majambazi watatu, ambapo awali walimteka Balozi wa nyumba kumi na kumpiga ili awapeleke kwa mlemavu huyo naye kwa kubaini nia mbaya akawapeleka nyumba
nyingine.
Akizungumza katika kituo cha kulelea yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Huruma kilicho chini ya kanisa katoliki, binti huyo Kulwa
Joseph amesema kuwa, watu ambao
hawakujulikana walivamia nyumbani kwa jirani na kuanza kuwapiga mjomba wake anayeishi nyumba ya jirani.
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw Saveli Maketa ambaye alimnusuru kwa kumhamisha porini walipokuwa wanaishi amesema kuwa hali ya
maisha ya walemavu wa ngozi wilayani humo inaonesha kuwa ni hatarishi ambapo amewataka wananchi kuwa na mshikamano ili kuwanusuru na
hali hiyo.
Mratibu wa chama cha wenye ulemavu mkoani Tabora Bw, Focus Magwesera amemtaja balozi alijeruhiwa na majambazi hayo kwa jina la Makoye Meli ambapo katika kutaka kumnusuru
mlemavu huyo, aliwapeleka majambazi hao kwa nyumba ya jirani, huku mwenyekiti wa walemavu wilaya ya Sirambo akitishiwa kuuawa.
Chapisha Maoni