0
Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema kuwa
amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari lake aina ya Volkswagen.

Bwana Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake ,alisema kuwabombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja wa dini ya
kiislamu katika eneo la uarabuni.

Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha hizobzitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais Mujika ambaye anajulikana kama Pepe anaishi katika shamba lake na hutoa pato lake kwa watu masikini.

Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari lake la Volkswagen Busqueda liliripoti kwamba ombi la gari hilo
lilifanywa katika mkutano wa kimataifa mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz Bolivia.

''Nilishangaa mara ya kwanza ,a hivyobasi nikapuzilia mbali.lakini baadaye ombi jengine lilikuja na hivyobasi nikaanza kulichukulia kuwa
swala la umuhimu'',. Alisema Mujika.

Chapisha Maoni

 
Top