0
TIMU ya Liverpool imeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Swansea usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Anfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Beki Mspanyola, Alberto Moreno aliifungia timu ya Brendan Rodgers bao la kwanza dakika ya 33, kabla ya Adam Lallana kufunga mawili dakika za 51 na 60 na Jonjo Shelvey kujifunga dakika ya 68 kuipatia Liverpool bao la nne.

Bao pekee la Swansea lilifungwa na Sigurdsson dakika ya 52 na sasa Liverpool inatimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 19, ingawa inabaki
nafasi ya nane.

Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Manquillo, Henderson, Lucas, Moreno, Lallana/Markovic dk77, Coutinho/ Borini dk89 na Sterling/Balotelli dk82.

Swansea; Fabianski, Richards/Rangel dk46, Fernandez, Williams, Taylor, Britton/Ki dk66, Shelvey, Dyer, Sigurdsson, Routledge na Bony/
Gomis dk62.

Chapisha Maoni

 
Top