MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 27 mpaka 30, ambaye jina lake halikufahamika mara moja,amekutwa akining'inia juu ya mti wa Mwembe uliopo katikati ya pori, nje kidogo ya mji wa Pongwe,Mkoani Tanga akidhaniwa kuwa amejinyonga.
Hali ya sintofahamu iliendelea kutanda
katika eneo hilo huku kila aliefika eneo hilo la tukio,alijikuta akipigwana butwaa na kustaajabu ya kuwa ni kipi kilichomsibu kijana yule wa makamo mpaka kufikwa na mauti ya aina ile.
Akizungumza mmoja wa mashuhuda wa
tukio hilo, kwa sharti la kutotaja jina
lake,alieleza kuwa ,walipata taarifa za
tukio hilo kutoka kwa kijana mmoja
aliekuwa akichunga ng'ombe katika pori
hilo, ambaye pia jina lake halikufahamika
mara moja,hali iliyowapelekea kwenda
moja kwa moja eneo la tukio kushuhudia
na kuona kama watamtambua mtu huyo
ama la,lakini kila aliefika kwenye tukio
hilo,hakuweza kumtambua huku wengine wakisema huenda mtuu huyo alikuwa ni mgeni kijijini hapo.
Ripota wetu aliyepo Jijini Tanga anaendele na juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo ili kuona kama anataarifa zozote juu ya tukio hilo.

Sehemu ya Wananchi wakazi wa Mji wa
Pongwe Mkoani Tanga wakiangalia mwili wa mtu huyo uliokuwa ukining'inia juu ya mti.Ambapo mpaka ripota wetu anaondoka eneo la tukio hakukuwa na Mwanausalama yeyote aliefika eneo hilo.

Chapisha Maoni