0
Usiku wa December 07 Tanzania imechukua tena headline kwenye vyombo mbalimbali vya habari
na hii ni baada ya Mtazania Idris kufanikiwa kushinda kwenye shindano la Big Brother Hot Shot 2014.

Mara baada ya Mshiriki wa Tanzania Katika Shindano la Big Brother Africa 2014 Idris Sultan kutangazwa mshindi, watanzania wengi walionekana kufurahishwa sana na Ushindi wake
huku wengine wakimpongeza kupitia kurasa zao za Twitter ...

Muda mfupi baadae Msanii Kutoka Nchini Nigeria Davido alionekana waziwazi kukerwa na Ushindi
huu wa Mtanzania Idris na kuamua kutweet "N They Cheat Again lol".
Tweet hii ilimfanya Msanii huyo wa Nigeria kushambuliwa kwa Maneno na watanzania wengi katika kurasa zao za twitter.

Usiku huo huo baada ya ushindi wa
Idris,Diamond naye aliibuka kidedea kwenye tuzo za The Future Awards Africa Prize in Entertainment 2014 zilizofanyika Lagos Nigeria usiku wa kuamkia leo na kuwatupilia mbali
wakali wengine wakiwemo Panshack au Ice Prince wa Nigeria na Michael Kwesi kutoka nchini Ghana.

Baada ya Ushindi huo, Diamond aliamua
kumjibu Davido kwa kuandika "Thanks God, we have cheated another one on the future Awards Africa in Lagos Nigeria…#Samenight Thank You
Allah" Ugomvi huo wa maneno haukuishia hapo tu,

Jokate Mwegelo ambaye ni X-Girlfiriend wa Diamond naye alitoa Onyo kali kwa Davido akimtaka aombe radhi kwa kauli yake:
“I think it’s wise that you give an apology. You don’t need Tanzanians hating you…” Aliandika
Jokate

Chapisha Maoni

 
Top