0
Kaka mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nicholaus amesimamia fumanizi la dada’ke ambaye ni mwanafunzi wa sekondari moja jijini Dar ambapo alimfumania chumbani na njemba
mmoja sharobaro aliyetajwa kwa jina la Abuu Ally, mkazi wa Mbagala-Charambe, Dar.

Akisimulia mkasa wa fumanizi hilo, Nicholaus alisema amekuwa akiumizwa na taarifa kwamba kila ikifika saa 2: 00 usiku kuna mwanaume amekuwa akijipenyeza na kuingia chumbani kulala
na mdogo wake wa kike kisha kuchomoka alfajiri.

Alidai kuwa kuwa mara nyingi vitendo hivyobhufanyika wikiendi . Ili kumnasa mwanaume huyo, Nicholaus aliandaa vijana kadhaa wa kazi kwa ajili ya
fumanizi na kisha akamtaarifu Mjumbe wa Mtaa wa Maji-Matitu, Hawa Ally kuwa wana kazi eneo lake hivyo akatoa ushirikiano uliofanikisha kumnasa Abuu.

Baada ya kukiri kosa mbele ya kiongozi huyo wa serikali za mtaa, pande zote zilikubali kusuluhishwa ambapo Abuu alikubali kulipa faini ya shilingi laki moja na kupewa muda wa siku moja kutekeleza adhabu hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top