Baadhi ya wananchi mkoani Kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba
na makazi na kuwaweka kiporo viongozi
wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakiongea na mwandishi mwetu, wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua nini hatima ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine waliohusika katika sakata hilo na kumuuondoa waziri Tibaijuka na pia wamebaki na sintofahamu ambapo wamemtaka Rais kutoa ufafanuzi kuwa licha ya kumng’oa madarakani
kiongozi huyo Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akaunti hiyo ya Tegeta Escrow au la.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kagera Hamimu
Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa wakati akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam kwa kumuondoa kiongozi huyo.
Kwa upande wake, katibu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo Chadema katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa
Pesa za Escrow zitarudishwa lini katika akaunti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho na kwamba pesa hizo hazirudishi?.
Kwa upande wake aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amesema licha ya Rais kumuondoa katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa amerudi jimboni kwake kwaajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi ya kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na
kwamba Pesa hizo alizopewa na Rugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama pesa hizo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow ndo maana hakutaka
kujiuzulu.
Chapisha Maoni