0
Mwigizaji wa filamu za kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar kujibu kesi ya kushambuliwa vijana wawili, Rashid Balazi na Juma Bushiri, wakazi wa jijini Dar.

Katika kujibu kesi hiyo, Madam Wema hatakuwa peke yake kwani mpambe wake, Petit Man naye anahusika katika kesi hiyo kwa kuwa ndiye mshtakiwa wa kwanza.

Hivi karibuni kabla Madam Wema hajasafiri kwenda nchini Ghana kufanya kazi na staa wa huko, Van Vicker, Petit Man alidaiwa kuhusika kuandaa mchezo mchafu wa kuwateka na kuwashushia kipigo cha mbwa mwitu Rashid na
Juma, tukio ambalo lilichukua nafasi nyumbani kwa Wema, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar.

Ilidaiwa kwamba, Petit Man alipoteza simu na kuwahisi vijana hao ambao mmoja wao alikuwa ni fundi bomba, ambaye alikuwa akitengeneza bomba nyumbani hapo.

Baada ya kuwabana vijana hao na kutotoshelezwa na majibu yao, ilidaiwa kwamba Petit Man, kwa kushirikiana na Wema waliwaita vijana wa kihuni
‘mbwa mwitu’ na kuwafungia nyumbani kwa Wema kisha kuwapa kipondo kizito ili watoe simu hiyo lakini hadi dakika za mwisho walikataa kuwa hawakuchukua.

Chapisha Maoni

 
Top