0
Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika
baadhi ya maduka.

Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia miundombinu
mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya
wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara.

Katika hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza uelekeo na kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya magari yakiingia kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria zime zama
katika maji na kulazimika kuvutwa.

Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa akizungumzia alalamiko hayo
ya wananchi hao amesema manispaa wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe kutupa taka kwenye mitaro na kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji kupoteza ueleko na
kujaa katika makazi ya wananchi.

Chapisha Maoni

 
Top