0

Cesc Fabregas alionyeshwa kadi nyekundu kwenye
mchezo wa kirafiki kati ya Chelsea na Liverpool
uliopigwa nchini Marekani, Chelsea ikiibuka na
ushindi wa bao 1-0.
Gary Cahil aliifungia Chelsea bao pekee la mchezo
huo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi.
Fabregas aliyemfanyia madhambi mchezaji mpya
wa Liverpool Ragnar Klavan, alikwenda kuomba
msamaha baada ya mpambano huo kumalizika.


Naye Antonio Conte kocha wa Chelsea aliomba
radhi na kudai kuwa uchovu ulipelekea Fabregas
kufanya rafu hiyo ambayo ilikuwa ya bahati
mbaya.
Timu hizo ziko nchini Marekani zikiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya
Uingereza unaotarajia kuanza Agosti 13.




Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top