0
Mkutano Mkuu wa wanachama wa klabu ya soka ya Simba uliopangwa kufanyika Julai 10, mwaka
huu katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Masaki,
jijini Dar es Salaam, umesogezwa mbele hadi Julai 31, mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Rais wa
klabu hiyo, Evans Aveva, ilieleza kwamba uamuziI wa kuahirishwa kwa mkutano huo umetokana na
sababu kubwa ya uongozi kutaka kuwajibika zaidi
kwa upande wa timu inayojiandaa na michuano ya
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Alisema uongozi umefanya mabadiliko hayo uweze
kuelekeza nguvu zake kukiandaa kikosi kwa ajili ya
mazoezi.
“Tunaomba radhi kwa wanachama kutokana na
usumbufu uliojitokeza, lakini tunakiri kwamba
mambo haya yanafanywa ili kuongeza ufanisi
ndani ya klabu yetu,” ilieleza taarifa hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top