matamko yenye mlengo wa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kauli hiyo ya tume imetolewa siku mbili baada ya
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai wa Zanzibar,
Kamishna Msaidizi Salum Msangi, kuwakataza
mawakili kuwawakilisha watuhumiwa katika kesi za
madai ya uvunjifu wa amani visiwani humo au
makosa yanayoashiria kufanyika kwa msukumo wa kisiasa.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Bahame Nyanduga,
alisema jana zuio hilo ni batili kwa kuwa ni kinyume cha sheria na misingi ya haki za binadamu.
Alisema wameshangazwa nas kusikitishwa na
tamko hilo la Kamishna Msangi na kwamba
haliendani na dhana ya utawala wa sheria na utawala bora.
Kwa mujibu wa Nyanduga, kila taasisi na kila mtu
anatakiwa kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya
mwaka 1977, Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984
na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya
Zanzibar Na. 7 ya mwaka 2004, pamoja na
mikataba ya kimataifa ya haki za kisiasa na kiraia
ya mwaka 1966 ambayo Tanzania imeridhia.
Alisema Ibara ya 13(6) ya Katiba ya tanzania na
kifungu cha 12 (6) cha Katiba ya Zanzibar, ambazo
zinaweka miongozo ya usimamizi wa haki,
ikiwamo ya kusikilizwa wakati wa upelelezi na
uendeshaji wa kesi za jinai mtu anapokuwa chini
ya ulinzi, lazima utu wake uheshimiwe.
Kadhalika, alisema kifungu cha 41 cha sheria ya
mwenendo wa jinai ya mwaka 2004 kinampa haki
Wakili aliyesajiliwa na mahakama Kuu,
kumwakilisha au kumshauri mtu yeyote
anayetuhumiwa au kushtakiwa kwa kosa lolote.
“Tume inazisisitiza mamlaka zote zenye
kusimamia upelelezi na kuendesha mashtaka
kutekeleza na kuheshimu matakwa ya Katiba na
sheria,” alisema.
Kuhusu hali ya uhasama iliyopo Zanzibar, Tume
ilisema ili maelewano yarudi kama ilivyokuwa awali
visiwani humo, ni vyema hatua za makusudi na
haraka zikafanyika, hususan kwa viongozi wa
kitaifa na vyama vyote vya siasa, vikiwamo CCM
na CUF, kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi wa
suluhisho la kudumu kwa ajili ya kuzuia matatizo
ya uvunjifu wa amani kujirudia.
Hatua nyingine, alisema ni taasisi zinazosimamia
ulinzi na usalama, likiwamo jeshi la polisi, vyombo
vya usalama na vyombo vingine vya dola kuwa
makini katika kufanya kazi kwa kufuata misingi ya
utawala bora, haki za binadamu na utawala wa
kisheria ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
“Tume imepokea kwa masikitiko taarifa ya vitendo
vya uhalifu na uvunjaji wa haki za binadamu
vinavyofanyika visiwani Zanzibar ikiwamo watu
kutengwa kutokana na itikadi za siasa hata
kuchangia kuvunjika kwa ndoa.
Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea kwa muda
mrefu tangu kufutwa kwa uchaguzi wa mwaka jana
na kufanyika ule wa marudio.
“Watu wanachomewa nyumba zao, wanabauguana,
hawashirikiani katika shughuli za kijami.
Kwa mfano baadhi ya watu wananyimwa usafiri
katika magari, kususiwa harusi, maziko na nyumba
za ibada, ndoa zinavunjika kutokana na wanawake
kukataa kutii amri za waume zao za kuwazuia
kushiriki uchaguzi wa marejeo.
Vitendo hivyo pamoja na vile vya kuchoma
nyumba ni kinyume cha haki za binadamu,” alisema.
Nipashe
Chapisha Maoni