0

Bao la Erick Lamera alilofunga kwa kichwa kipindi
cha pili liliinusu Totenham Hotspurs isipate kipigo
kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya
Uingereza dhidi ya Everton.
Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1, Everton ikiwa
ya kwanza kufunga kupitia kwa Ross Barkley,
ulikuwa ni mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa
moja wavuni.
Spurs ilifanya vizuri sana msimu uliopita, ni timu
inayoundwa na kikosi cha vijana zaidi na huenda
msimu huu ikafanya vizuri kutokana ubora wa
kocha wake Pochetinno pamoja na vijana hao
wenye uchu wa mafanikio.
Msimu uliopita ilimaliza nafasi ya tatu nyuma ya
Arsenal, itashiriki ligi ya mabingwa Ulaya msimu
huu sambamba na Leicester, Arsenal na Man City
inayoanzia hatua ya mtoano.
Mchezo huo uliopigwa Goodison Park ulikuwa na
upinzani wa aina yake, Everton sasa inaongozwa
na Koeman, kocha wa zamani wa Southampton
sawa na Pochetinno aliyetokea Southampton pia.
Matokeo mengine ya michezo ya EPL iliyopigwa
leo, siku ya ufunguzi;




Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top