0

Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga Leo Uwanja
wa Taifa Jijini Dar es Salaam
kurudiana na Mo Bejaia ya Algeria katika Mechi ya
Kundi A la KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF CC
ambayo ni lazima washinde ili kuweka uhai
matumaini yao finyu ya kusonga Nusu Fainali.
Yanga wapo wakiwa mkiani mwa Kundi A wakiwa
na Pointi 1 tu baada Mechi 4 wakati
Vinara ni TP Mazembe ya Congo DR wenye Pointi
10 wakifuatiwa na MO Bejaia ya Algeria yenye
Pointi 5 na Medeama wana Pointi 5 baada ya zote
kucheza Mechi 4 na kubakisha 2.
Kundi B limebakisha Mechi 1 tu na tayari FUS de
Rabat ya Morocco na ES Sahel ya Tunisia
zimeshatinga Nusu Fainali.
Katika Kundi A, Yanga wamefungwa Mechi 3 na
Sare 1 na katika Mechi ya kwanza na MO Bejaia
huko Algeria walilala 1-0.
Wakati Yanga wakicheza na MO Bejai, TP
Mazembe wako Ugenini kucheza na Medeama.
Refa wa Mechi hii ni kutoka Ethiopia, Bamlak
Tessema Weyesa, akisaidiwa na Kindie Mussie na
Temesgin Samuel Atango.
Mwamuzi wa Nne ni Haileyesus Bezezew Belete,
wakati Kamishna ni Gaspard Kayijuka wa Rwanda.
Na Msimamizi wa Mechi ni Isam Shaaban kutoka
Sudan.




Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top