MSIMU MPYA wa Soka wa Ligi Kuu huko England
umeanza Leo huko Kingston upon Hull, KCOM
Stadimu, kwa Timu iliyopanda Daraja Hull City
kuwakaribisha Mabingwa wa England Leicester
City kwa kuwatandika Bao 2-1.
Safari hii Ligi hii haina tena Jina la Mdhamini na
itajulikana rasmi kama Ligi Kuu tofauti na Msimu
uliopita ilipoitwa Barclays Premier League
kutokana na udhamini wa Barclays.
Hull City, ambao hawana Meneja wa kudumu
baada ya Steve Bruce kuamua kuondoka na wapo
chini ya Msaidizi wa zamani wa Sir Alex Ferguson,
Mike Phelan, walienda Mapumziko wakiwa Bao
1-0 mbele kwa Bao ambalo lilifungwa Dakika za
Majeruhi baada ya krosi ya Robert Snodgrass
kupigwa Kichwa na Curtis Davies na Kipa wa
Leicester Kasper Schmeichel kuokoa na Mpira
kugombewa na Wachezaji Wawili wa Hull, Abel
Hernandez na Adama Diomande, wote wakiwania
kupiga Tikitaka na Mpira kutinga wavuni.
Hata hivyo, Bao hilo alipewa rasmi Adama
Diomande.
Kipindi cha Pili Dakika ya 47 Mabingwa Leicester
walisawazisha kwa Penati ya Riyad Mahrez
iliyotolewa kufuatia Rafu ya Huddlestone kwa Gray
ambayo hakika ilifanyika nje ya Boksi.
Hull City walikwenda 2-1 mbele katika Dakika ya
57 kwa Bao nzuri la Robert Snodgrass la Shuti la
chini kufuatia kizaazaa Goli mwa Leicester
kilicholetwa na Krosi ya Ahmed Elmohamady na
kuokolewa fyongo na Fulbeki Danny Simpson na
kumdondokea Snodgrass aliemaliza vizuri.
Hadi mwisho Hull City 2 Leicester City 1.
Robert Snodgrass akishangilia bao lake dakika ya
57 kipindi cha bao alilolifunga kwa shuti kali
Dama Diomandé bao la kwanza dakika ya (45'+1')
kafunga.
Robert Snodgrass dakika ya (57') Huku bao la
Leicester City ambao ni Mabingwa watetezi
likifungwa kwa mkwaju wa penati na Riyad Mahrez
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni