0

Lionel Messi amefuta uamuzi wake wa kustaafu
kuichezea Timu ya Taifa ya Argentina,
Messi, mwenye Miaka 29, aliamua kustaafu
kuichezea Nchi yaka mara tu baada ya kutolewa
na Chile kwenye Fainali ya Copa America Mwezi
Juni huko USA.
Kwenye Fainali hiyo, Messi alikosa Penati kwenye
Mikwaju ya Penalti Tano Tano na kuifanya
Argentina ishindwe kutwaa Taji katika Fainali za
Mashindano makubwa Manne katika Miaka 9.
Messi, ambae ameifungia Argentina Bao 55 katika
Mechi 133, ametwaa Taji 1 tu akiichezea Nchi
yake na hilo ni Medali ya Dhahabu kwenye Fainali
za Michezo ya Olimpiki ya Mwaka 2008.
Jana Messi aliteuliwa kuwemo kwenye Kikosi cha
Argentina cha kucheza Mechi za Kanda ya Nchi za
Marekani ya Kusini za kufuzu kucheza Fainali za
Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
zitakazochezwa dhidi ya Uruguay na Venezeula
mwanzoni mwa Septemba.
Mara baada ya kugeuza uamuzi wake wa kustaafu,
Messi ameripotiwa kusema amerejea tena
kuichezea Argentina kwa sababu ya mapenzi kwa
Nchi yake na Jezi ya Argentina.
Messi ametajwa kwenye Kikosi hichon cha
Argentina ambacho kitakuwa chini ya Meneja
Mpya Edgardo Bauza na Wachezaji kutoka
England ambao wamo humo ni Watatu wa Man
City Sergio Aguero, Pablo Zabaleta na Nicolas
Otamendi, Wawili wa Manchester United Sergio
Romero na Marcos Rojo, Ramiro Funes Mori wa
Everton na Erik Lamela wa Tottenham.
Messi yumo humo Kikosini pamoja na mwenzake
wa Klabu yao FC Barcelona ya Spain Javier
Mascherano wakifanya Jumla ya Wachezaji 27
Kikosini.



Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top