Simba wanamtuhumu Kessy kwamba alianza
kushiriki shughuli za Yanga kabla mkataba wake
na klabu ya Simba haujamalizika.
Wanamtuhumu kushiriki mazoezi na shughuli
nyingine ikiwemo ile ya tarehe 25 May siku ya
Jumatano kwenye mchezo wa fainali ya kombe la
FA ambapo Yanga ilicheza na Azam.
Kessy alikuwa upande wa Yanga na mbali na hapo
alifanya mazoezi na klabu ya Yanga kwa mujibu
wa Simba ikiwa tarehe 15 ya mwezi June bado
haijafika (siku ya kumalizika kwa mkataba wake).
Baada ya fainali hiyo Simba wanaendelea
kumtuhumu Kessy kuendelea na mazoezi na klabu
ya Yanga, wanasema kwamba, kati ya tarehe 12
June siku tatu kabla ya mkataba wake kumalizika,
alisafiri na Yanga kwenda Uturuki ambapo Yanga
ikwenda kupiga kambi kwa ajili ya maandalizi ya
mechi za nane bora za kombe la shirikisho.
Aidha TFF wamesisitiza kuwa Yanga hawawezi
kumtumia mchezai huyo kwenye michuano ya
shirikisho kwa kuwa Simba hawajatoa barua ya
kumruhusu(release letter).
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni