Kwa mujibu wa mtandao wa SalehJembe,
Shirikisho la Soka la Kimataifa, FIFA limefungua
tena dirisha la usajili kwa saa 48.
Taarifa kutoka ndani ya TFF zinasema dirisha hilo
la usajili litafungwa Jumapili saa 6 usiku, kwenda
Jumatatu na hii ni nafasi kwa klabu ambazo
hazikuwasilisha usajili kukamilisha.
Mabingwa wa Tanzania, Yanga pamoja na Coastal
Union pia African Lyon zilikuwa kati ya timu za
Ligi Kuu Bara na Daraja la Kwanza ambazo
hazikuwa zimekamilisha usajili.
Hii inaweza kuwa nafasi ya klabu hizo kumalizana
na suala hilo ili kutulia na kulenga maandalizi ya
mwisho kabla ya kuanza Ligi Kuu Bara, wiki ijayo.
Posted: 👉👉 ⚽ Africa News Sports
Chapisha Maoni