kundi A Jumamosi Oktoba 8, kutakuwa na mchezo kati ya Pamba ya Mwanza na
Polisi Dar kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam es Salaam wakati
African Sports itakuwa mwenyeji wa Kiluvya United kwenye Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo ya Daraja la Kwanza itaendelea Jumapili Oktoba 9, 2016 kwa mchezo
utakaozikutanisha Ashanti United na Friends Rangers; zote za Dar es Salaam.
Kadhalika Jumatatu, kutakuwa na mchezo kati ya Mshikamano ya Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa. Mchezo huo, pia
utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Kurugenzi ya
Iringa na Coastal Union ya Tanga ufakaofanyika huko Mufindi ukifuatiwa
na michezo mitatu siku ya Jumapili Oktoba 9 ambayo Mlale itacheza na Majimaji ya Songea huko Uwanja wa
Majimaji Njombe Mji itaikaribisha Kemondo wakati KMC itacheza na Mbeya
Warriors kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Kundi C; Jumamosi Oktoba 8, mwaka huu Mvuvumwa ya Kigoma itacheza na Stand
United ya Singida wakati Panamo itapambana na Alliance huku Polisi
Dodoma itacheza na Polisi Mara wakati Jumapili Rhino ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT ya Tanga.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni