Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa haina
inachokihitaji zaidi ya pointi tatu ambazo
zitawafanya kufikisha pointi 29 na kufikisha
ushindi wa 11 kwa kocha Omog
Kikosi cha kocha Joseph Omog kesho Jumapili
kitashuka kwa mara nyingine kwenye uwanja wa
Uhuru kusaka pointi tatu dhidi ya timu dhaifu ya
Toto African kutoka Jijini Mwanza.
Simba inayoongoza ligi ikiwa na pointi 26,
inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo
kutokana na mwenendo wa wapinzani wao Toto
kutokuwa na mwenendo mzuri huku wakiwa
nafasi ya mwisho kutoka mwisho kwenye
msimamo wakiwa na pointi nane.
Inaweza kuwa ni mechi ya kupumzisha baadhi ya
wachezaji nyota kwa Omog, baada ya kazi nzito
waliyofanya Alhamisi iliyopita dhidi ya Mbao FC,
ambayo walilazimika kujihakikishia kuondoka na
pointi tatu dakika za lala salama ingawa wageni
hao hawakupewa nafasi ya kutoa upinzani huo.
Winga Shizza Kichuya pamoja na kumaliza
dakika zote 90, lakini hakuweza kufanya chochote
sawa na Laudit Mavugo aliyeanzishwa kipindi
cha kwanza baada ya kuanzia benchi mechi mbili
zilizopita lakini alitolewa kipindi cha pili na nafasi
yake kuchukuliwa na Fredrick Blagnon.
Kiungo Muzamiru Yasini mfungaji wa bao pekee
lililowapa pointi tatu Simba dhidi ya Mbao
anatarajiwa kuanza sambamba na Ibrahim Ajibu
na pengine kocha akamuanzisha Blagnon baada
ya kiwango kizuri alichokionyesha mchezo
uliopita.
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa haina
inachokihitaji zaidi ya pointi tatu ambazo
zitawafanya kufikisha pointi 29 na kufikisha
ushindi wa 11 kwa kocha Omog tangu aanze
kuifundisha timu hiyo kwenye mechi za ligi ya
Vodacom msimu huu.
Kipa Vicent Angban ataendelea kuanza kikosi cha
kwanza akisaidiwa na Mohamed Hussein na
Janvier Bukungu na kwenye ulinzi wa kati
wakianza Juuko Murshid aliyefanya vizuri mechi
iliyopita pamoja na Mzimbabwe Method Mwanjali.
Kwaupande wao Toto African wameshawasili Dar
es Salaam, lakini matarajio ya ushindi yakiwa
madogo ingawa hii ni moja ya timu
inayoasumbua sana Simba.
Msimu uliopita Toto iliweza kuvuna pointi nne
mbele ya timu hiyo baada ya kulazimisha sare ya
kufungana bao 1-1 kwenye uwanja wa CCM
Kirumba na katika mchezo wa marudiano
uliopigwa Dar es Salaam Toto alishinda bao 1-0.
Kwa rekodi ya msimu uliopita na siku za nyuma
Simba wanatakiwa kuingia kwenye mchezo huu
wakiwa na tahadhari kubwa kwani Toto pamoja
na kuwa na migogoro lakini inapokwenda
kukutana na Simba inabadilika na kuwa timu
hatari kwao.
Mshambuliaji Wazir Junior atabaki kwenye
kumbukumbu za mashabiki wa Simba pamoja na
kocha Jackson Mayanja ambao walishudia timu
yao ikipoteza mwelekeo wa kutwaa ubingwa kwa
bao lake zuri la mbali dakika ya 26.
Mbali ya Waziri lakini Toto wanasafu kali ya
ushambuliaji inayomjumuisha Lusajo Leriants
hivyo pamoja na matatizo waliyokuwa nao lakini
mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani na
Simba wanalazimika kupambana ili kuvunja
rekodi mbaya pindi wanapokutana na timu hiyo
kutoka Jijini Mwanza.
Matokeo yeyote ya kufungwa au kutoka sare
yanaweza kuwa mabaya kwa Toto na kuzidi
kuiweka kwenye nafasi mbaya ya kushuka daraja
kwani hivi sasa ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi
nane lakini ushindi utakuwa mzuri kwa Simba
ambayo niwazi msimu huu imekusudia kutwaa
ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya kutaabika
kwa misimu minne nyuma.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni