Real Madrid imepata sare ya nne mfululizo katika
michuano yote baada ya leo kulazimishwa sare ya
bao 1-1 na Eibar katika mchezo wa ligi kuu ya
Hispania, La Liga Santender.
Fran Rico alikuwa wa kwanza kuipatia Eibar bao la
kuongoza bao ambalo lilirejeshwa na Real Madrid
dakika kumi baadae kupitia kwa Gareth Bale.
Atletico Madrid imeilaza Valencia mabao 2-0 na
kuiondosha Real Madrid kileleni kwenye msimamo
wa La Liga.
FC Barcelona inayo nafasi ya kushika usukani
kwenye msimamo wa ligi hiyo kama itapata
ushindi dhidi ya Celta.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni