0

FC Barcelona imeendeleza uteja kwa Celta Vigo
baada ya Jumapili usiku kukubali kipigo cha
mabao 4-3 katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania,
La Liga Santander.
Celta ilijipatia mabao matatu ndani ya dakika 10
kupitia kwa Sisto na Iago Aspas huku Jeremy
Matheau akijifunga.
Mpaka mapumziko Celta ilitoka kifua mbele kwa
mabao hayo matatu.
Kipindi cha pili Barca inayocheza bila nyota wake
Lionel Messi aliye majeruhi, iliweza kupata mabao
matatu, mawili yakifungwa na Gerrard Pique na
moja likipachikwa na Neymar kwa mkwaju wa
penati.
Aidha, makosa ya mlinda mlango wa Barca, Te
Stegan yaliizawadia Celta bao la nne baada ya
mpira aliojaribu kumpasia Jordi Alba kumgonga
Pablo Hernandez na kutinga wavuni.
Matokeo hayo yanaisukuma Barca hadi nafasi ya
nne kwenye msimamo wa ligi, wangeweza kukwea
kileleni kama wangepata ushindi kwenye mchezo
huo.
Atletico Madrid inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi
15 sawa na Real Madrid.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top