0

Mabingwa wa soka kwa ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati timu ya Azam FC, jana
imeshindwa tena kuvuna point 3 katika mchezo wa
ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la
Chamazi, Dar es Salaam, kwa kulazimishwa sare
ya 2-2 na Ruvu Shooting.
Ruvu Shooting walikuwa wa kwanza kupata bao
kupitia kwa Fully Maganga katika dakika ya 8 ya
mchezo, na Azam kufanikiwa kusawazisha dakika
ya 29 kupitia kwa Baptista Mugiraneza kwa kichwa
akimalizia kona ya Mcha na kufanya timu hizo
kwenda mapumziko zikiwa sare ya 1-1 .
Kipindi cha pili kilianza kwa Azam kutawala zaidi
mchezo na kufanikiwa kupata bao la pili katika
dakika ya 70 kupitia kwa Khamis Mcha kwa shuti
akitumia vema pasi ya kichwa ya Shaban.
Wakati Azam wakidhani kuwa wamemaliza kazi,
Shaaban Kisiga akaisawazishia Ruvu Shooting bao
dakika za mwishoni na kufanya matokeo hadi
mwisho wa mchezo kuwa sare ya 2-2 na timu
zote kugawana point.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha point 11
katika michezo 7 iliyocheza ikiwa nafasi ya 4
nyuma ya Yanga yenye point 12.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top