0

Timu ya Majimaji ya Songea imeendelea kuwa
shamba la bibi kwa kugawa point baada ya jana
kupigwa mabao 2-0 na Stand United katika uwanja
wake wa nyumbani wa Majimaji mjini Songea.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara umeifanya
Majimaji kupoteza mchezo wa 7 mfululizo huku
ikiwa haina point hata moja, na hivyo kuendelea
kushika mkia katika msimamo wa ligi hiyo.
Mchezo huu ni kwanza kwa kocha Kally Ongala
ambaye alirejeshwa kuinoa klabu hiyo baada ya
kuona mwenendo wake ukiwa wa kusuasua.
Matokeo hayo yanaifanya Stand United kuzidi
kujiimarisha zaidi katika msimamo wa ligi kuu
ikifikisha point 15 nyuma ya vinara Simba yenye
point 17, na kulinda rekodi yake ya kutopoteza
mchezo wowote kati ya michezo saba tangu
kuanza kwa ligi.
Katika mechi nyingine, Mbao FC imelazimishwa
suluhu ya 0-0 na JKT Ruvu katika dimba la CCM
Kirumba, huku Mtibwa Sugar ikiichapa African
Lyon bao 1-0 katika dimba la Manungu, Morogoro.
Mbeya City imeifunga Mwadui FC bao 1-0 Sokoine
Jijini Mbeya na Kagera Sugar imeitandika Tanzania



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top