Yanga imeanza kwa kasi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwafunga wenyeji wao Ngaya de Mbe ya Comoro mabao 5-1
Kikosi cha Yanga kimeanza kwa kasi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwafunga
wenyeji wao Ngaya de Mbe ya Comoro mabao
5-1.
Kipigo hicho kinaifanya Yanga kuwa na kazi
nyepesi katika mchezo wa marudiano ambao
utapigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam
Jumamosi ijayo.Wawakilishi hao wa Tanzania
katika michuano hiyo mi kubwa Afrika
walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa
mabao mawili yaliyofungwa na kiungo Mzambia
Justine Zullu na winga Simon Msuva.
Zullu akilifunga bao lake la kwanza tangu atue
Yanga dakika ya 43, akimalizia kazi nzuri ya
Simon Msuva na wakati mashabiki wa Ngaya de
Mbe wakiamini watakwenda mapumziko wakiwa
nyuma kwa bao moja Msuva alifunga bao la pili
dakika ya 45 kazi nzuri ya Haruna Niyonzima.
Yanga ilirudi kwa kasi kipindi cha pili na
iliwachukua dakika 9 kufunga bao la pili mfungaji
akiwa Mzambia Obrey Chirwa ambaye alimalizia
kazi nzuri ya Msuva.
Dakika ya 65 Amissi Tambwe aliifungia Yanga
bao la nne baada ya kazi nzuri iliyofanywa na
Niyonzima na kuwakatisha tamaa wenyeji wao
Ngaya.
Ngaya walionekana kuzidi kupambana wakitafuta
angalau bao la kufutia machozi na jitihada zao
zilizaa matunda dakika ya 66 baada ya Said
Anfane kufunga bao zuri akimalizia krosi
iliyochongwa kutoka winga ya kushoto mwa
lango la Yanga.
Baada ya kufungwa bao hilo Yanga walikuwa juu
na kuanza kulisakama lango la Ngaya ambapo
dakika ya 73 Thabani Kamusoko alifunga bao la
pili baada ya kupokea pasi nzuri ya Juma
Mahadhi aliyeingia muda fupi kuchukua nafasi ya
Tambwe.
Mchezo huo uliendelea kwa timu zote
kushambuliana hasa Yanga ambao alipoteza
nafasi mbili za wazi katika dakika za 78 na 80
ambapo Mahadhi alishindwa kutumia na
kuzitumia nafasi hizo.
Hadi filimbi ya mwisho Yanga iliibuka na ushindi
huo mnono ambao sasa itahitaji nguvu kidogo
katika mchezo wa marudiano ili kusonga mbele
raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni