0

Manchester City imecheza mchezo wa tano bila
kupata ushindi katika michuano yote baada ya
kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Southampton
kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza(EPL)
uliopigwa katika dimba la Etihad Jumapili jioni.
Southampton ilikuwa ya kwanza kupata bao la
kuongoza, Redmond akitumia vyema makosa ya
John Stone aliyerudi mpira nyuma bila ya
kuangalia.
City iliyotawala mchezo huo ilipata bao la kufutia
machozi kwenye dakika ya 55 kipindi cha pili
baada ya Iheanacho kupasia wavuni krosi ya Sane.
Aidha mapema kabla ya bao hilo, John Stone
alifunga bao ambalo hata hivyo lilikataliwa na
mwamuzi, kwa kuwa Sergio Aguero aliyejaribu
kufunga kabla ya Stone alikuwa ameotea.
City imefikisha pointi 20 sawa na Arsenal na
Liverpool iko kileleni kutokana na kuwa na uwiano
mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top