0

Mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain huenda akashiriki katika mechi dhidi ya Leicester City Licha ya kuondoka katika uwanja wa Wembley
baada ya mechi ya Jumapili ya FA akiuguza jeraha.
Kiungo huyo wa kati aligongwa katika mguu lakini kcha Arsene Wenger anasema kuwa alichukua
hatua ya tahadhari.
Mchezaji wa Leicester Wes Morgan anauguza jereha la mguu huku msimu wa Nampalys Mendy
ukikamilika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.
Beki Robert Huth anarudi baada ya kuhudumia marufuku ya ligi ya klabu bingwa ,lakini Slimani
anaendelea kuuguza jeraha.


Chapisha Maoni

 
Top