Mamelodi Sundowns ya
Afrika Kusini wamepangwa
Kundi C katika Ligi ya
Mabingwa Afrika pamoja na
Esperance ya Tunisia, AS Vita
ya Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC) na Saint-
George ya Ethiopia.
Katika droo iliyopangwa leo
mjini Cairo, Misri yalipo
makao makuu ya Shirikisho
la Soka Afrika (CAF),
mabingwa mara nyingi zaidi
wa Kombe hilo, Al Ahly ya
Misri waliotwaa taji hilo mara
nane katika miaka ya 1982,
1987, 2001, 2005, 2006,
2008, 2012 na 2013
wameangukia Kundi D.
Vigogo hao wa Misri
wamepangwa pamoja na
mabingwa wa mwaka 1992,
Wydad Athletic Club ya
Morocco, Coton Sport ya
Cameroon na Zanaco ya
Zambia.
Zamalek ya Misri wanaofuatia
Ahly kutwaa marab nyingi
taji hilo, wakiwa wamebeba
mara tano sawa na TP
Mazembe ya DRC,
wamepangwa Kundi B
pamoja na USM Alger ya
Algeria, Ahli Tripoli ya Libya
na Caps United ya
Zimbabwe.
Kundi A lina timu za Etoile
du Sahel ya Tunisia
mabingwa wa mwaka 2007,
vigogo wa Sudan, El Hilal na
El Merreikh na mabingwa wa
Msumbiji, Ferroviario Beira.
Katika Kombe la Shirikisho,
KCCA ya Uganda imepangwa
Kundi A pamoja na FUS
Rabat ya Morocco, Club
Africain ya Tunisia na Rivers
United ya Nigeria.
Mabingwa watetezi TP
Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) wamepangwa Kundi D
pamoja na Supersport United
na Afrika Kusini na Horoya
AC ya Guinea na CF Mounana
ya Gabon.
CS Sfaxien imepangwa Kundi
B pamoja na Platinum Stars,
MC Alger na Mbabanwe
Swallows wakati Zesco
United ya Zambia imepangwa
Kundi C pamoja na
Recreativo do Libolo ya
Angola, Al Hilal Elobeid ya
Sudan na Smouha ya Misri.
Chapisha Maoni