Yanga Clement Sanga ametolea
ufafanuzi kuhusiana na Suala kupeleka
Timu ya Vijana kwenye mchezo wa
Kirafiki dhidi ya Combine ya Jeshi kwa
ajili ya Kusherehesha Maazimisho Ya
miaka 53 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.
Sanga amesema walifanya kitendo
hicho kwa maslahi mapana ya Yanga
Kwani wanakabiliwa na michezo mingi
hasa ile ya Ligi na Nusu fainali ya
Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbao
FC.
-Kwa kifupi uamuzi wa kutokupeleka
kimoso cha kwanza nikwa maslahi
mapana ya yanga katika kufanya vizuri
mashindano tunayoshiriki, lakini Pia
kulikuwa na dosari kadhaa katika
kufikia makubaliano ya ushiriki wa
mechi hiyo hasa upande wa stahiki ya
yanga , upana wa kikosi, ukaribu wa
mechi ya FA na Ligi Pia , hivyo
niwaombe wanachama na wapenzi wa
yanga kuwa wavumilivu hasa katika
kipindi hiki cha mpito' Alisema.
Nawaomba Radhi.
Pia Sanga amewaombe radhi wote
waliosikitishwa na uamuzi huo, japo
amekitaja kitendo hicho cha kupeleka
timu ya vijana chini ya umri wa miaka
20 kuwa ni uamuzi wenye manufaa
kwa klabu hiyo.
-Niwaombe tushikamane tuwe kitu
kimoja , kuelekea kutwaa makombe
tunayoshiriki kwa sasa, na kuendelea
kuichangia fedha yanga timu
tuipendayo' Aliongeza.
Ufafanuzi huo Unakuja muda Mfupi tu
baada ya Waziri wa Habari, Sanaa,
Utamaduni na Michezo Dkt Harrison
Mwakyembe kuomba kukutana na
uongozi wa Yanga ili kupata maelezo
ya kina ya kitendo hicho cha kitapeli
ambacho Yanga wamekifanya.
Chapisha Maoni