0
MSHAMBULIAJI wa kimataifa
wa Tanzania, Mbwana Ally
Samatta jana ametokea
benchi KRC Genk ikiibuka na
ushindi wa 3-0 dhidi ya
Kortrijk kwenye mchezo wa
Kundi B kuwania tiketi ya
kucheza michuano ya UEFA
Europa League mwakani.
Samatta aliingia dakika ya 66
kwenda kuchukua nafasi ya
mfungaji wa bao la kwanza la
Genk jana, kinda Mbelgiji,
LeandroTrossard aliyefunga
kwa penalti dakika ya 14
katika mchezo huo ambao
mabao mengine yalifungwa
na kinda mwingine Mbelgiji,
Siebe Schrijvers mawili,
dakika ya 45 na 70.
Mbwana Samatta akimtoka
mchezaji wa Kortrijk kwenye
mchezo wa jana
Samatta alianzia benchi jana
baada ya mchezo uliopita
kuanzishwa Jumatano, lakini
hakufunga KRC Genk
wakilazimishwa sare ya 1-1
na wenyeji, AS Eupen Uwanja
wa Kehrweg mjini.
Genk inaendelea kuongoza
Kundi B katika mchuano wa
kuwania tiketi ya Europa
League kwa pointi zake 16
sasa baada ya kucheza
mechi sita na Samatta jana
ameiichezea Genk mechi ya
55 tangu ajiunge nayo
Januari mwaka jana kutoka
TP Mazembe ya DRC akiwa
amefunga mabao 18.
Kati ya mechi hizo 55,
michezo 18 Samatta alicheza
msimu uliopita na 37 msimu
huu na kati ya hiyo, ni
michezo 33 tu ndiyo alianza,
10 msimu uliopita na 23
msimu huu.
Mechi 21 kati ya hizo
alitokea benchi, nane msimu
uliopita na 13 msimu huu,
wakati 11 hakumaliza baada
ya kutolewa, tano msimu
uliopita na sita msimu huu
na katika mabao hayo 18, 12
amefunga msimu huu na sita
msimu uliopita.
Kikosi cha Genkkilikuwa;
Ryan, Nastic, Colley,
Dewaest, Castagne, Berge/
Malinovskyi dk73, Heynen,
Writers, Trossard/Samatta
dk66, Buffalo na Naranjo/
Boëtius dk81.
KV Kortrijk : Kaminski,
Goutas, De Smet/Ivanof
dk65, Chevalier, Van Der
Bruggen, Rougeaux, Rolland,
Ouali, Totovytskyi D'Haene
na Sarr/Stojanovic dk45.

Chapisha Maoni

 
Top