msimu huu, baada ya
kutupwa nje ya michuano ya
Kombe la Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), inayojulikana
kama Azam Sports
Federation Cup (ASFC)
kufuatia kipigo cha 1-0
kutoka kwa Mbao FC katika
mchezo wa Nusu Fainali jioni
ya leo Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza.
Mapema mwanzoni mwa
msimu, Yanga ilivuliwa taji la
Ngao ya Jamii baada ya
kufungwa na Azam FC kwa
penalti 4-1 kufuatia sare ya
1-1 katika mchezo wa
kuashiria ufunguzi wa msimu
mpya, Agosti 17, mwaka
jana.
Na sasa Yanga ina jukumu la
kutetea taji lake moja
lililobaki na kubwa zaidi, la
Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara ambako
wanakabana koo na
wapinzani wao wa jadi,
Simba SC.
Katika mchezo wa leo
uliochezeshwa na refa Erick
Onoka wa Arusha,
aliyesaidiwa na Julius Kasitu
na Mdogo Makame wa
Shinyanga hadi mapumziko,
tayari Mbao walikuwa mbele
kwa bao hilo 1-0.
Ni Yanga wenyewe
waliojifunga bao hilo dakika
ya 27, baada ya beki wake,
Andrew Vincent ‘Dante’
kuunganishia nyavuni kwake
krosi ya Pius Buswita katika
harakati za kuokoa.
Mbao walibadilisha mfumo
wa uchezaji baada ya bao
hilo na kuanza kucheza kwa
kujihami, jambo ambalo
liliwasumbua Yanga.
Kipindi cha pili, Mbao
walifanikiwa kuendekea
kuwabana Yanga na kujilinda
vyema hatimaye kuandika
historia ya kuwa timu ya
kwanza ya Mwanza na ya nje
ya Dar es Salaam kwa ujumla
kufika fainali ya Kombe la
TFF.
Na sasa Mbao FC watakutana
na Simba SC katika fainali ya
michuano hiyo baadaye
mwezi huu Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam. Simba
iliwatoa washindi wa pili wa
msimu uliopita, Azam FC kwa
1-0 jana, bao pekee la
Mohammed Ibrahim.
Kikosi cha Mbao FC kilikuwa;
Benedict Haule, David
Mkwasa, Alex Ntiri, Boniface
Maganga, Salmin Hoza,
Yussuf Ndikumana, Jamal
Mwambeleko, George
Sangija, Everigustus Bernard/
Robert Ndaki dk73, Pius
Buswita na Ibrahim Njohole.
Yanga SC; Deogratius
Munishi ‘Dida’, Hassan
Kessy/Juma Abdul dk67,
Mwinyi Mngwali, Andrew
Vicent ‘Dante’, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Said Juma
‘Makapu’/Geoffrey
Mwashiuya dk46, Simon
Msuva, Thabani Kamusoko,
Obrey Chirwa/Emmanuel
Martin dk83, Amissi Tambwe
na Haruna Niyonzima.
Chapisha Maoni