0
SIMBA SC inaweza kurejea
kileleni mwa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara leo,
iwapo itawafunga wenyeji,
Mbao FC katika mchezo
utaaofanyika Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza.
Wekundu hao wa Msimbazi
wanaingia katika mchezo wa
leo, wakitokea Geita
walipoweka kambi ya wiki
moja wakitokea Bukoba,
ambako Jumapili iliyopita
walifungwa 2-1 na wenyeji
Kagera Sugar na kuangukia
nafasi ya pili kwenye
msimamo wa Ligi.
Mabingwa watetezi, Yanga SC
ambao Jumamosi iliyopita
waliifunga 1-0 Azam FC
ndiyo waongoza Ligi Kuu
kwa sasa kwa pointi zao 56
baada ya kucheza mechi 25
wakiwazidi pointi moja tu
Simba ambao leo wanacheza
mechi ya 26.
Mshambuliaji tegemeo wa
Simba, Mrundi Laudit
Mavugo ataiongoza timu
yake leo dhidi ya Mbao FC
Katika mchezo wa leo, Simba
itamkosa beki wake wa kati,
Abdi Banda ambaye
amesimamishwa kwa muda
usiojulikana kucheza Ligi Kuu
kwa kosa la kumpiga ngumi
kiungo wa Kagera Sugar,
George Kavilla katika mchezo
wa ligi hiyo baina ya timu
hizo Aprili 2, Uwanja wa
Kaitaba Bukoba.
Maamuzi hayo hayo
yaliyofikiwa kwenye kikao
cha Kamati ya Usimamizi na
Uendeshaji wa Ligi Tanzania
au Kamati ya Saa 72 Ijumaa
mjini Dar es Salaam ni
chungu kwa Simba, kwani
tayari inamkosa beki wake
wa kati tegemeo, Mzimbabwe
Method Mwanjali, ambaye ni
majeruhi.
Maana yake, kwa vyovyote
leo kocha Mcameroon,
Jopseh Marius Omog
atalazimika kuwapanga
Novaty Lufunga na Juuko
Murshid na kwenye benchi
hatakuwa na mchezaji wa
akiba wa katikati.
Simba SC itamkosa pia
Nahodha wake, Jonas Mkude
kwa sababu ya kadi za njano
wakati habari njema tu ni
kwamba, beki wa kulia,
Mkongo Janier Besala
Bokungu anarejea baada ya
kumaliza kutumikia adhabu
yake ya kadi nyekundu
aliyoonyeshwa katika mchezo
dhidi ya mahasimu, Yanga
Februari 25.
Mchezo mwingine wa Ligi
Kuu leo ni kati ya wenyeji,
Mtibwa Sugar na Azam FC
Uwanja wa Manungu Turiani,
Morogoro.
Mechi za juzi Kagera Sugar
ililazimishwa sare ya 0-0 na
JKT Ruvu Uwanja wa Kaitaba,
Bukoba, Ndanda FC ilishinda
2-1 ugenini Uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya dhidi ya
wenyeji Mbeya City na Maji
Maji ililazimishwa sare ya
1-1 na African Lyon mjini
Songea mkoani Ruvuma,
wakati jana Stand United
iliichapa 1-0 Tanzania
Prisons Uwanja wa
Kambarage, Shinyanga.

Chapisha Maoni

 
Top