0
KLABU ya TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrsia ya
Kongo (DRC) jana iliibuka na
ushindi wa 2-0 dhidi ya JS
Kabylie ya Algeria katika
mchezo wa kwanza wa
mchujo wa kuwania tiketi ya
kucheza hatua ya makundi ya
Kombe la Shirikisho
mjini Lubumbashi.
Mabao yote ya mabingwa
hao watetezi wa Kombe la
Shirikisho yalifungwa na
wageni Uwanja wa Mazembe,
la kwanza Mzambia Nathan
Sinkala dakika ya 11 na la
pili Salif Coulibaly kutioka
Mali dakika ya 90.
Mabingwa mara tatu wa
Kombe la Shirikisho, ambayo
ni rekodi, CS Sfaxien ya
Tunisia walipata ushindi wa
2-1 ugenini dhidi ya Rail
Kadiogo nchini Burkina Faso.
Club Africain ilikamilisha
ubabe wa timu za Tunisia
kwa kuichapa 2-1 AS Port
Louis nchini Mauritius,
mabao ya Slimene Kchok na
Mannoubi Haddad.
Zesco United ya Zambia
walitoka nyuma kwa mabao
mawili na kutoa sare ya 2-2
na Enugu Rangers ya Nigeria
huku Patrick Kongolo
akisawazisha dakika ya 76.
Chibuzor Madu alifunga kwa
penalti kipindi cha kwanza
bao la Rangers na Osas
Okoro akafunga la pili kwa
"Flying Antelopes" baada tu
ya mapumziko.
Mkenya beki David Owino
akafunga bao lake la pili
kwenye mashindano ya
mwaka huu kwa Zesco,
ambayo mwaka jana ilitolewa
Nusu Fainali ya Mabingwa.
SuperSport United ya Afrika
Kusini ilitoa sare ya 1-1 na
Barrack Young Controllers
nchini Liberia wakati
Platinum Stars ilifungwa 2-0
na AS Tanda nchini Ivory
Coast.
Mapema juzi, KCCA
iliwaangusha Al Masry kwa
bao 1-0 Uwanja wa Philipo
Omondi mjini Kampala,
Uganda.

Chapisha Maoni

 
Top