kwa mabao 2-0 na kushinda
3-2 dhidi ya wenyeji, Mbao
FC katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara jioni ya leo Uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza.
Sifa zimuendee mshambuliaji
Muivory Coast, Frederick
Blagnon aliyetokea benchi na
kwenda kufunga mabao
mawili dakika za lala salama
kabla ya kiungo Muzamil
Yassin kufunga la ushindi.
Katika mchezo huo
uliochezeshwa na refa
Shomari Lawi kutoka
Kigoma aliyesaidiwa na
Joseph Bulali na Mohammed
Mkono wote wa Tanga,
dakika 45 za kipindi cha
kwanza zilimalizika wenyeji
Mbao FC wakiwa mbele kwa
mabao 2-0.
George Sangija alianza
kuwainua vitini mashabiki wa
timu ya nyumbani kwa bao
safi dakika ya 21 baada ya
kuwatoka mabeki wa Simba
na kuingia kwenye boksi la
Simba kabla ya kumchambua
kipa Peter Manyika.
Baada ya bao hilo, kocha
Mcameroon wa Simba,
Joseph Marius Omog alifanya
mabadiliko akimpumzisha
mshambuliaji Pastory
Athanas na kumuingiza
kiungo Said Hamisi Ndemla.
Mbao wakaendelea kutawala
mchezo baada ya bao hilo na
haikuwa ajabu dakika ya 36
walipopata bao la pili kupitia
kwa Evarigestus Bernard
aliyemalizia pasi ya mfungaji
wa bao la kwanza, Sangija.
Baada ya bao hilo, kocha
Omog wa Simba akamuinua
mshambuliaji Mrundi Laudit
Mavugo kwenda kuchukua
nafasi ya beki wa kulia,
Hamad Juma.
Simba wakafanya mabadiliko
ya ndani, Bokungu akienda
kucheza beki ya kulia na
Mghana James Kotei akirudi
kucheza beki ya kati na
Mganda Juuko Murshid.
Kipindi cha pili, kocha Omog
alikianza na mabadiliko tena
akimtoa mshambuliaji Juma
Luizio na kumuingiza
Blagnon aliyekwenda kufanya
kazi kubwa akicheza mechi
yake ya kwanza ya Ligi kuu
mzunguko wa pili.
Blagnon alifunga bao la
kwanza la Simba dakika ya
82 kwa kichwa kuparaza
akiwa amelipa mgongo lango
la Mbao kufuatia mpira mrefu
wa James Kotei.
Bao hilo lilifungwa dakika
tano tu baada ya Nahodha
wa Mbao, Yussuf Ndikumana
kuumia na kukimbizwa
hospitali, nafasi yake
ikichukuliwa na.
Blagnon tena akawainua
vitini mashabiki wa Simba
baada ya kufunga katika
purukushani kwenye eneo la
Mbao kufuatia mpira mrefu
wa Bokungu dakika ya 91.
Katika mchezo huo uliodumu
kwa dakika 103, kiungo
Muzamil Yassin aliifungia
Simba bao la ushindi dakika
ya 96 akimalizia mpira
uliorudi baada ya kuokolewa
na mabeki wa Mbao.
Ushindi huo unairejesha
Simba kileleni, ikifikisha
pointi 58 baada ya kucheza
mechi 26, wakati mabingwa
watetezi, Yanga wanarudi
nafasi ya pili kwa pointi zao
56.
Kikosi cha Mbao FC kilikuwa;
Erick Ngwengwe, Asante
Kwasi, David Mwasa,
Boniphace Maganga, Yussuf
Ndikumana, Vincent Philipo,
George Sangija, Salmin Hoza,
Pius Buswita, Ibrahim
Njohole na Everigeston
Bernard.
Simba SC; Peter Manyika,
Hamad Juma, Mohammed
Hussein ‘Tshabalala’,
Juuko Murshid, Janvier
Bokungu, James Kotei, Shiza
Kichuya, Muzamil Yassin,
Juma Luizio, Mo Ibrahim na
Pastory Athanas.
Chapisha Maoni