0
Timu ya Toto África imeendelea
kujiweka katika mazingira magumu
baada ya kukubali kichapo cha mabao
mawili kwa bila kutoka kwa Azam Fc
katika mchezo ambao umefanyika
Ijumaa kwenye uwanja wa Azam
Complex, Dar Es Salaam.
Mchezo ulianza kwa Kasi timu zote
zikionekana kutafuta bao lá mapema.
Mshambuliaji wa Azam Shabaan Iddi
aliwaweka kufua Mbele wenyeji hao
kwa kufunga bao la mapema katika
dakika ya 13 bao ambalo lilionekana
kuvuruga mipango ya
Wakishamapanda hao wa kutoka Jijini
Mwanza.
2-0
 Hadi mapumziko Azam 1-0 Toto
Áfricans,Kipindi cha pili timu zote
zilirejea zikiwa zimejipanga upya lakini
Azam walionekana kujipanga zaidi
dakika ya 51 mshambuliaji Ramadhan
Singano akaongeza bao la pili
,matumaini ya Toto kupata hata goli la
kuvutia machozi hayakuzaa matunda
huku mshambuliaji Waziri Junior
akikosa nafasi kadha Za wazi katika
mchezo huo ambao Azam
walionekana kuumiliki.
Alama 29
Kufuatia matokeo hayo Toto Africans
wanabaki katika nafasi ya 14 wakiwa
na alama 29 wakiwa wamebakiwa na
michezo miwili dhidi ya Mtibwa Sugar
na Yanga SC. Não Azam Fc wako
katika nafasi ya tatu wakiwa na alama
52.

Chapisha Maoni

 
Top