Timu ya Mbao FC Ya kutoka Jijini
Mwanza, imesafiri kuelekea Bukoba
Mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo
dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika
Jumapili kwenye uwanja wa Kaitaba.
Akizungumza na futaa.co.tz wakati
wakiondoka Msemaji wa Klabu ya
Mbao Klisant Malinzi amesema timu
hiyo imefanya maandalizi ya kutosha na kuwa wako tayari kukabiliana na Wakata Miwa hao wa Kagera Maarufu kama Wanankurukumbi. Tumejiandaa
-Maandalizi yako vizuri wachezaji
wako vizuri hatuna nakesha na
tunamatumaini tutashinda huo
mchezo ili kupata pointi tatu muhimu, hatuko Salama sana tunahitaji ushindi ni mchezo mgumu lakini tutajitahidi kushinda" amesema Malinzi.
Aidha Malinzi ameeleza sababu
zilizowafanya kupoteza dhidi ya Azam na kusema kuwa Kocha tayari
ameyafanyia kazi mapungufu yao.
-Mchezo wa Azam tulipoteza kwa
kuwa safu yetu ya Ulinzi ilikuwa na
mapungufu lakini hilo mwalimu
amelifanyia kazi na nina matumaimani
mambo yatakuwa vizuri" ameongeza
Malinzi.
Alama 30
Mbao ambao wako katika nafasi ya 12
Wakiwa na alama 30 Wanahitaji
kupata ushindi ili kuimarisha nafasi
yao katika msimamo wa Ligi hiyo.
Kwa upande wao Kagera Sugar ambao wako katika nafasi ya nne wakiwa na alama 47 alama 2 nyuma ya Azam walio katika nafasi ya tatu wanahitaji ushindi ili kutimiza ndoto yao ya kumaliza katika nafasi ya tatu bora msimu huu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni