Uhsindi Mnono wa Mabao 4-2 dhidi
ya Mwadui FC katika mchezo
uliofanyika kwenye uwanja wa
Manungu Complex, Turiani Mkoani
Morogoro.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa
na Ally Makarani aliyefunga bao la
mapema katika dakika ya 1 ya
mchezo, Huku Stamily Mbonde
akifunga mabao mawili katika dakika
ya 4 na 72 na bao la nne la Mtibwa
limefungwa katika dakika ya 59 na
Salehe Hamis.
Aidha Mabao ya Kufutia machozi ya
Wachimba Almas Mwadui FC
yamefungwa Baada ya Beki wa Mtibwa
Sugar Kasiani Ponela Kujifunga
alipokuwa akiokoa hatari langoni
mwake, na lingine likifungwa na Salim
Hamis dakika ya 87.
Uwanja kujaa maji.
Mchezo ambao uliochezeshwa na
Mwamuzi Mbaraka Rashid kutoka
Jijini Dar es Salaam ulikosa radha
kutokana na Uwanja wa Manungu
kujaa maji na matope yaliyowafanya
kushindwa kulitandaza soka la
Kitabuni.
Matokeo hayo yanawafanya Mwadui
FC kusaliwa na alama 35, huku
wakibakiwa na mchezo wa mwisho
dhidi ya Mnyama Simba SC, Wakati
Mtibwa Sugar wao waking’ang’amia
mafasi ya Tano wakiwa na alama 41.
JKT Ruvu 0-1 Majimaji.
Kwingineko Katika dimba la CCM
Mkwakwani Jijini Tanga, Maafande wa
JKT Ruvu Wameumana vilivyo na
Wanalizombe Majimaji ya Songea na
mchezo huo kumalizika kwa Majimaji
kufufua matumaini ya kubaki kwenye
ligi baada ya kutembeza kichapo cha
bao 1-0, bao ambalo limefungwa na
Kelvin Sabato.
Matokeo hayo yanawafanya Majimaji
kufikisha alama 32 na kukwea hadi
bafasi ya 11 ya msimamo wa ligi kuu
soka Tanzania bara huku JKT Ruvu
ambao tayari wameshuka daraja
wakishika nafasi ya mwisho kwa
kukusanya alama 23.
Tanzania Prisons 2-1 Ndanda FC.
Katika Uwanja wa kumbukumbu ya
Sokoine Jijini Mbeya Wajelajela
Tanzania Prisons wawameibuka na
ushindi dhidi ya Wanakuchele Ndanda
FC wa mabao 2-1, na kufifisha ndoto
za Ndanda kucheza ligi kuu soka
Tanzania bara msimu ujao.
Kwani kwa kichapo hicho ndanda
wanashuka hadi katika nafasi ya 14
wakiwa na alama 30 huku wakibakiwa
na mchezo mmoja pekee, wakati
Tanzania Prisons wanachumpa hadi
nafasi ya nane baada ya kujikusanyia
alama 34 katika michezo 29.
Chapisha Maoni