0
Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva
ameishukuru Kampuni ya Kubashiri ya
Sportspesa kutoka nchini Kenya kwa
kuidhamini Timu hiyo na kusema
udhamini huu utasaidia pakubwa
kuimarisha klabu hiyo nje na ndani ya
uwanja.
 Aveva amesema udhamini huo
utakuwa chachu kwa maendeleo ya
timu hiyo kufanya vizuri.
Utaleta maendeleo
-Udhamini huu utakuwa chachu kwa
mafanikio yetu nje na ndani ya
uwanja, tumekuwa tukikabiliwa na
matatizo ya ufinyu wa bajeti jambo
ambalo limekuwa likitufanya wakati
mwingine kushindwa kufanya vizuri,
amesema Aveva.
Aidha Aveva amesema udhamini huo
utaisaidia pakubwa timu hiyo kufikia
hadhi ya kimataifa.
Kusajili
 -Hatua hii itatuwezesha Simba kutoa
ushindani tutaweza pia kusajili
wachezaji wenye uwezo mkubwa na
kufanikisha malengo yetu ya kuwa
miongoni mwa vilabu bora barani,
ameongeza Rais huyo wa Simba.
Aidha Simba wamepata udhamini
wenye thamana ya Bilioni 4 kwa
kipindi cha miaka mitano kutoka kwa
kampuni hiyo ya Bahati Nasibu ya
kutoka Nchini.

Chapisha Maoni

 
Top