0
Ligi Kuu soka Tanzania Bara
imeendelea tena ambapo Mjini Bukoba
Wanankurukumbi Kagera Sugar
wamewaalika Wagumu Mbao Fc,
Katika Uwanja wa Kaitaba na
kushuhidia Kagera wakilizamisha
Jahazi la Mbao FC kwa kuwachapa
mabao 2-1.
Mabao ya Ally Nasoro ndiyo yalitosha
kuwapa ushindi Kagera Sugar licha ya
Mbao Fc Kutangulia mapema Katika
dakika ya 13 kwa bao la George
Sangija.
Penati Mbao wanakosa.
Aidha katika mchezo huo Mbao
watajilaumu wenyewe kwani,
walizawadiwa penati , baada ya
George Sangija kufanyia madhambi
katika eneo la Hatari, lakini Bonidace
Maganga akashindwa Kumfunga
mlinda Mlango Juma Kaseja baada ya
kuupangua na kuwa Goal Kick.
Kipigo hicho kinawafanya Mbao FC
kuwa katika hatari kubwa ya kushuka
Daraja kwani wapo katika Nafasi ya 13
wakiwa na alama 30 huku wakibakiwa
na mchezo mmoja pekee ambao
watacheza na Mabingwa Watetezi
Yanga Mei 20 Jijini Mwanza.

Chapisha Maoni

 
Top