wamezidi kuchanja Mbuga kuuelekea
Ubingwa wa tatu Mfululizo wa ligi kuu
soka Tanzania baada ya kuibuka na
ushindi Kiduchu wa mabao 2-1 dhidi
ya Mbeya City.
Katika mchezo huo uliofanyika katika
uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
Yanga ndio waliokuwa wakwanza
kupata bao katika dakika ya 7 ya
Mtanange huo kupitia kwa Kiungo
Mshambuliaji Simon Msuva ambaye
amefunga bao lake 14 msimu huu.
Aidha Dakika chache baada ya bao
hilo, Simon Msuva alitolewa nje na
nafasi yake kuchukuliwa na Juma
Abdul kufuatia majeraha ya kichwa
aliyoyapata baada ya kugongana na
Mchezaji wa Mbeya City Tumba Lui.
Kipindi cha pili.
Hadi timu zinakwenda Mapumziko
Yanga walikuwa wakiongoza kwa Bao
1-0, na kipindi cha pili kilipoanza
Mbeya City walikuja kasi na kufanikiwa
kupata bao la Kusawazisha kupitia
kwa Haruna Shamte katika dakika ya
57.
Bao hilo halikudumu sana kwani
Mnamo dakika ya 65, Mshambuliaji wa
Kimataifa wa Yanga Obrey Chirwa
akafunga bao la pili baada ya pasi ya
Geofrey Mwashiuya, na kuifanya Timu
yake Kuvuna alama Tatu Muhimu na
kurudisha kisasi cha kufungwa na
Mbeya City katika mzunguko wa
Kwanza.
Msimamo.
Ushindi huo unawafanya Yanga
Kusogea Kileleni wakiwa na alama 65
sawa na Mnyama Simba lakini
wakibakiwa na Michezo miwili wakati
Simba wakibakiwa na mchezo Mmoja
pekee.
Chapisha Maoni