wenye umri wa chini ya
miaka 17 Tanzania, maarufu
kama Serengeti Boys,
Jumatatu itapambana na
Black Starlets ya Ghana
kwenye mchezo wa kirafiki
wa kimataifa utakaofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Katika mchezo huo
utakaoanza saa 10.00 jioni,
Serengeti Boys itautumia
kama ni ishara ya kuwaaga
mamilioni ya Watanzania
kabla ya kusafiri kwenda
kwenye fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa vijana
zitakazofanyika Gabon
kuanzia Mei 14, mwaka huu.
Lakini kabla ya kutua Gabon,
Serengeti Boys itakwenda
Rabat, Morocco kufanya
kambi ya takribani mwezi
mmoja kuanzia Aprili 5,
mwaka huu. Ikiwa huko
angalau itacheza mechi za
kirafiki zisizopungua mbili
dhidi ya wenyeji morocco na
timu nyingine ya jirani ama
Tunisia au Misri.
Kambi hiyo ya Morocco
itamalizika Mei mosi, mwaka
hu ambako timu itasafiri hadi
Cameroon.
Ikiwa Cameroon, timu
itacheza mechi mbili za
kirafiki za kimataifa dhidi ya
wenyeji yaani Mei 3 na 6,
mwaka huu kabla ya kusafiri
Mei 7, mwaka huu kwenda
Gabon ambako Serengeti
Boys imepangwa kundi B
pamoja na timu za Mali,
Niger na Angola.
Vipimo vya mechi dhidi ya
Ghana kadhalika hapo
baadaye Cameroon, vitakuwa
mwafaka kwenye kufanya
tathmini ya uwezo wa
Serengeti Boys kwani
wapinzani hao wamekuwa na
rekodi nzuri kwenye soka la
vijana na kwa kipindi hiki
zimepangwa kundi A pamoja
na wenyeweji Gabon na
Guinea.
Kila la kheri Serengeti Boys
katika mapambano ya
kuwania ubingwa wa Afrika
kadhalika kucheza fainali za
Kombe la Dunia hapo
Novemba, mwaka huu
zitakazofanyika India.
Serengeti Boys inaweza na
Mtanzania tunakuomba
kuichangia timu hii kwa
namna ya 223344 kupitia
mitandao yote ya simu.
Chapisha Maoni