0
Waziri wa Habari,utamaduni sanaa na michezo Dr
Harrison Mwakyembe amewaomba watanzania
wajitokeze kwa wingi katika kuhakikisha wanasaidia
timu ya soka ya Serengeti boys.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na
www.wapendasoka.com akiwa katika ziara wilayani
Kwimba jijini Mwanza, Dr. Mwakyembe alisema
watanzania waiunge mkono Serengeti boys ili
Iweze kucheza kombe la Mataifa ya Afrika kwa
vijana nchini Gabon baada ya hapo waweze kufuzu
kwajili ya kucheza kombe la Dunia la vijana nchini
India mwezi wa 11 mwaka huu.
Mheshimwa Dr. Mwakyembe alisema ana imani
kubwa na timu hiyo kuwa itafanya vyema na
ameahidi kuendelea kuisapoti.
Aidha Waziri Mwakyembe ameipongeza pia timu ya
taifa 'Taifa stars" kwa matokeo mazuri waliyopata
dhidi ya Botswana na Burundi hivi karibuni.
Waziri Mwakyembe ameziomba sekta binafsi
kuhakikisha zinachangia katika kuinua elimu ya
michezo.Pia waziri huyo alisema kamati ya ufundi
zimedidimiza sana soka nchini kutokana na
mambo yao ya kuamini sana katika mambo ya
ushirikiana kuliko kufanya mazoezi.

Chapisha Maoni

 
Top