kocha Albert Stuivenberg alifunga goli lake
dakika ya 72 likiwa ni goli la pili kwa timu yake
Mbwana Samatta jana ameifungia bao moja
timu yake, KRC Genk ikishinda 4-0 Uwanja wa
Luminus Arena mjini Genk dhidi ya Lokeren
katika mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza
UEFA Europa League msimu ujao.
Samatta alifunga bao lake dakika ya 72, likiwa
la pili katika mchezo huo baada ya Alejandro
Pozuelo kutangulia kuifungia Genk la kwanza
dakika ya 45 kabla ya Jean-Paul Boetius
kufunga la tatu dakika ya 77 na Jose Naranjo
kumalizia la nne dakika ya 90.
Bao hilo linamfanya Samatta aliyecheza mechi
hiyo akitoka nyumbani kuichezea timu yake ya
taifa, Taifa Stars na kuufunga mabao yote
katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana
Jumamosi iliyopita, afikishe mabao 18 katika
mechi 49 alizoichezea Genk tangu asajiliwe
Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya
DRC.
Genk inaongoza Kundi B lenye timu sita ikiwa
na pointi 3 sawa na Kortrijk huku timu zote (6)
zikiwa zimecheza mechi moja. Genk inaongoza
kundi kwa tofauti ya wastani wa magoli.
Chapisha Maoni